Head image
Govt. Logo

Hits 30553 |  1 online

     
Kuhusu Wizara

Wizara ya Katiba na Sheria imeundwa mnamo tahere 3/3/2019, baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein, kufanya maamuzi ya kuigawa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kufanya Wizara mbili. Kutokana na Mgawanyiko huo, Wizara ya Katiba na Sheria inayo majukumu Yafuatayo:

MAJUKUMU YA WIZARA

 1. Kuandaa na kusimamia mipango, sera, sheria na tafiti zinazohusiana na Katiba na Sheria
 2. Kusimamia shughuli za utawala, uendehaji na utumishi katika Wizara
 3. Kusimamia utekelezaji wa Katiba ya Zanzibarna ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
 4. Kusimamia Shughuli za Mhimili wa Mahakama
 5. Kusimamia shughuli za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
 6. Kusimamia shughuli za Mkurugenzi wa Mashtaka
 7. Kusimamia shughuli za Tume ya Kurekebisha Sheria
 8. Kuratibu na kusimamia shughuli za ofisi za Mufti
 9. Kuratibu na kusimamia shughuli za kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana
 10. Kuratibu shughuli za Wizara Pemba

DIRA

Kutoa huduma bora kwa jamii kwa kuzingatia misingi ya Katiba, sheria, haki, demokrasia na utawala bora.

DHAMIRA

Kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora kwa jamii zenye ufanisi na tija kwa kuzingatia misingi ya Katiba na Sheria, haki za binadamu ili kuwa na Mfumo Madhubuti wa Kufanikisha Mipango ya Maendeleo ya Taifa

TUNU/ MISINGI YA THAMANI

 1. Umoja katika utoaji wa huduma
 2. Kutokuwa na ubinafsi katika utoaji wa huduma
 3. Uadillifu/ uaminifu
 4. Kuzingatia haki/utii wa sheria
 5. Kuzingatia masuala ya jinsia
 6. Mashirikiano, uwajibikaji na uwazi
 7. Ufanisi na tija
 8. Huduma bora na kuwajalii wataka huduma
 9. Kuzingatia matokeo
 10. Thamani halisi ya pesa (value for money)
 11. Utunzaji wa siri

MUUNDO WA WIZARA

Wizara ya Katiba na Sheria inaundwa na Taasisi zifuatazo:-

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe WaziriTel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz