USAJILI WA WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA
Posted: 2020-02-21 05:03:24
Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar kupitia Idara ya Msaada wa Kisheria inawatangazia Watoaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria kuwa, Mfumo wa usajili wa Watoaji wa Huduma za Kisheria kwa njia ya Kielektroniki umeanza kazi rasmi .
Kwa mujibu wa Sheria Nam.13 ya 2018 kifungu cha 4(1)(C) Kinawataka Watoaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria Kujisajili. Huduma za Usajili inapatikana kupitia Tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria www.sheriasmz.go.tz Ingia katika sehemu ya Huduma ya Msaada wa Kisheria.