TANGAZO KUTOKA OFISI YA MUFT ZANZIBAR.
Posted: 2020-03-26 12:27:27
Assalaam Alaykum.
Ndugu Wakuu wa Vyombo vya Habari na Wananchi kwa ujumla
Ofisi ya Mufti Zanzibar itasoma Dua maalum kuiombea Nchi yetu kupitia ZBC TV na Redio, Kesho Ijumaa saa 1:00 usiku Inshaallah. Dua hiyo itaongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Kaabi, Wakuu wa Vyombo vya Habari wanaombwa kuwasiliana na Uongozi wa ZBC ili waweze kuipata Dua hio kikamilifu na kuirusha kupitia vyombo vyao vya Habari kama Televisheni, Redio, Gazeti na Mitandao ya Kijamii.
Wananchi wote wanaombwa wafuatilie na kujumuika katika kisomo hicho kupitia Televisheni na Redio zao .
Tuungane pamoja kushirikiana Kuiombea Nchi yetu.
Ahsante
Othman M.Saleh
Kny: Katibu wa Mufti
Zanzibar