Hits 55958 | 1 online
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala bora Tanzania Jaji Mathew Pauwa Mhina amewataka viongozi na maafisa wa Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar kuendeleza ushirikiano na Tume hiyo ili kuondosha changamoto kwa pamoja za wananchi zinazo husiana na uvunjifu wa haki za binaadamu.

Ameyasema hayo wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar na Tume hiyo kuhusu utekelezaji wa majukumu mbali mbali ya tume hiyo ili kuweka uwazi kwa Serikali pamoja na Wizara ziweze kufahamu mambo yanayotekelezwa na Tume hiyo.
Amesema Wizara ya Katiba na Sheria moja ya jukumu iliyopewa ni kushughulikia haki za binaadamu sawa na Tume hiyo hivyo wanapowasiliana na kufanya kazi kwa pamoja itarahisisha kuondoa matatizo wanayoyapata wanannchi yanayohusiana na uvunjifu wa haki za binaadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.
Aidha ameongezea kuwa kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia kuboresha na kuondosha mkinzano kati ya tume hiyo na Wizara juu ya taarifa mbali mbali kabla kuwasilishwa katika vyombo vya kutunga sheria.
Naye, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar mh, Khamis Juma Mwalim ameahidi kuendeleza ushirikiano na Tume hiyo na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uzalendo ili kuhakikisha malengo ya serikali yaliyokusudiwa kwa tume hiyo yaweze kufikiwa.
Aidha amewataka kufanya kazi kwa umakini Zaidi kwa kuzigatia maslahi ya nchi.