Head image
Govt. Logo

Hits 27295 |  1 online

     
Mkutano wa siku mbili wa kukusanya maoni kwa ajili ya rasimu ya mtaala na muongozo wa kufundishia Wasaidizi wa Sheria Zanzibar.
news phpto

Mkutano wa siku mbili wa kukusanya maoni kwa ajili ya rasimu ya mtaala na muongozo wa kufundishia Wasaidizi wa Sheria Zanzibar.

Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar kupitia Idara ya Msaada wa Kisheria imekusanya maoni ya wadau mbali mbali kutoka Vyuo vya Elimu, Wizara ya Elimu, Mahakama ya Kadhi, wanasheria, watoaji msaada wa kisheria pamoja na jumuiya za wasaidizi wa kisheria kwenye kikao cha pamoja cha kujadili Rasimu ya Mtaala na Muongozo wa kufundishia wasaidizi wa Kisheria. Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mazizini tarehe 13-14 Machi 2020 wadau walipata fursa ya kuipitia kwa kina Rasimu ya Mtaala na Muongozo wa kufundishia Wasaidizi wa Sheria iliyowasilishwa na Ndugu Abdalla M. Mussa.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Bi Hanifa Ramadhan Said amewataka wadau walioshiriki katika kikao hicho kujadili na kutoa maoni yao kwa lengo la kuimarisha Rasimu ya Mtaala na Muongozo wa kufundishia Wasaidizi wa Sheria.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz