Hits 69507 | 4 online
Marehemu Mhe Abubakar Khamis Bakary aliteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar mwaka 2010-2015 katika kipindi cha awamu ya saba chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe Dkt Ali Mohamed Shein.
Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar imepokea kwa huzuni na mshituko taarifa ya kifo cha Mhe Abubakar Khamis Bakary.
Marehemu Abubakar Khamis Bakary pamoja na majukumu mengine aliyowahi kupitia ikiwemo nyadhifa mbalimbali kutumikia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 1984-1988.
Aidha baada ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Marehemu Mhe Abubakar Khamis Bakary aliteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar mwaka 2010-2015 katika kipindi cha awamu ya saba chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe Dkt Ali Mohamed Shein.
Marehemu Abubakar Khamis Bakary alizaliwa tarehe 02/11/1951 katika kijiji cha Mzambarauni Takao Wete Pemba na kufariki tarehe 11/11/2020 na kuzikwa Kianga Wilaya ya Magharibi 'A' Unguja
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi AMIN.