Head image
Govt. Logo

Hits 27033 |  1 online

     
Afisa Mdhamini Wizara ya Katiba na Sheria Pemba, Mattar Zahor Masoud.
news phpto

Afisa Mdhamini Wizara ya Katiba na Sheria Pemba, Mattar Zahor Masoud amesema ili kuwepo na ufanisi katika kazi ni wajibu wa kila mfanyakazi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa kufuata sheria kanuni na miongozo ya kazi.

Afisa Mdhamini Wizara ya Katiba na Sheria Pemba, Mattar Zahor Masoud amesema ili kuwepo na ufanisi katika kazi ni wajibu wa kila mfanyakazi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa kufuata sheria kanuni na miongozo ya kazi

Mattar amesema ni wajibu wa watendaji kufanya kazi kwa mashirikiano na kuacha tabia iliyojengeka kwa baadhi ya wafanyakazi kupikiana majungu badala yake wawe wabunifu na watekelezaji wazuri wa majukumu ya kazi

Afisa Mdhamini huyo alieleza hayo, alipokuwa akifungua mafunzo kwa watendaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, kuhusiana na kanuni ya utumishi wa umma ya mwaka 2014, yaliofanyika kwenye ukumbi Gombani Chakechake Pemba.

Alisema msingi imara kwa wafanyakazi ni kujenga mashirikiano ya pamoja ya kiutendaji kazi kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa, kuwa wazalendo wa kweli jambo ambalo litapelekea kuwepo uwajibikaji mzuri kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa umma

“ ni wajibu wangu kwenu kuwaona watendaji mnatekeleza majukumu yenu kwa ufanisi kwa kufuata taratibu za kiutendaji na kujenga misingi imara ya utawala bora hasa sehemu zenu za kazi hivyo naomba niwasisite kuzisoma na kuzifahamu kanuni za utumishi wa umma na kuacha kufanya kazi kwa mazowea ” alisisitiza Afisa Mdhamini

Aidha Ndugu Mattar amefafanua kuwa uwepo wa kanuni ya utumishi wa umma ya mwaka 2014, ni hatua moja, na hatua ya pili ni kwa wafanyakazi wote, kuisoma na kuifahamu ilivyo.

Mapema akiwasilisha mada ya kuhusu Kanuni ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2014 wakili wa kujitegemea Pemba, Suleiman Omar Suleiman amesema Kanuni ya utumishi imebainisha kuwa, kila taasisi ya umma italazimika kumfanyia tathmini ya utendaji wa kazi mtumishi wake kila mwaka, ambapo fomu ya tathmini itatolewa na Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

Katika kuimarisha utawala bora na utawala wa sheria, ni wajibu wa kila mtumishi kuzingatia majukumu yake ya kazi kwa kufuata muongozo na kanuni za utumishi wa Umma ili kumjengea mustakabali mzuri wa baadae katika kupata haki

Bikombo Hamad Rajab ni mmoja kati ya washiriki wa mafunzo hayo na amesema mafunzo hayo ya kukumbushwa wajibu na haki zao, kupitia Kanuni ya utumishi wa umma ya mwaka 2014, ni jambo jema kikazi na kuwaomba wafanyakazi wenzake kuhakikisha wanayafanyia kazi mafunzo hayo, ili wawe chachu ya maendeleo ya Wizara na Taasisi zake .

Nae Maryam Haji Mbarouk ameushukuru uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuona ipo haja ya kuwapatia mafunzo wafanyakazi wake na kuahidi kuyafanyia kazi, aidha kwa niaba ya washiriki wameomba kuwepo muendelezo wa mafunzo hayo ambayo yanasaidia kuamsha ari ya kuitendaji

“Mafunzo haya ni mazuri kwetu sisi wafanyakazi, maana lazima tukumbushwe juu ya sheria na kanuni za utumishi, hivyo lazima niupongeze uongozi wa Wizara yetu,’’alieleza.

Miongoni mwa vifungu vilivyomo kwenye Kanuni hiyo ni kile cha 87(1) ambacho kimetamka kuwa, mtumishi wa umma atakayepangiwa kazi katika mazingira hatarishi, atalazimika kulipwa posho, kama muongozo utakavyotolewa kutoka Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz