Head image
Govt. Logo

Hits 27819 |  4 online

     
Ndani ya Miaka 9 ya Uongozi wa Dkt Shein, Wizara ya Katiba na Sheria inajivunia kuwepo kwa Utawala Bora , Utawala wa Sheria na Demokrasia.
news phpto

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Mwalim amesema Wizara ya Katiba na Sheria inatekeleza misingi imara ambayo imeainishwa ndani ya Katiba ya Zanzibar.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Khamis Juma Mwalim amesema Wizara ya Katiba na Sheria inatekeleza misingi imara ambayo imeainishwa ndani ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, iliyoweka bayana kuwa Zanzibar itasimamiwa chini ya Utawala wa Sheria.

Hayo ameyaeleza wakati alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Televisheni ZBC TV Karume House katika kipindi maalum cha miaka 9 ya Uongozi wa Dkt Shein ambacho kilirushwa hewani pia na ZBC Redio Rahaleo .

Mhe Khamis amesema kuwepo kwa Amani na utulivu ndani ya miaka 9 ya uongozi wa Dkt Shein ni mafanikio tosha katika awamu hii ya saba inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Dk. Ali Mohammed Shein ambae anaitekeleza na kuisimamia vyema Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Kwa vipindi tofauti vya uongozi wa Dkt Shein Wizara ya Katiba na Sheria katika utekelezaji wa majukumu na mikakati yake inajivunia mafanikio mengi yakiwemo Usimamizi wa Sekta ya Sheria na Usimamizi wa Upatikanaji wa Haki.

Tume ya Kurekebisha Sheria, imeendelea kuzipitia Sheria na kuzifanyia mapitio Sheria 37, ambapo sheria 22 zimekamilika na kuwasilishwa katika mamlaka husika baadhi ya Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana namba 2/2007.

Sheria ya Mahusiano Kazini namba 1/2005, Sheria ya Ajira namba 11/2005, na Sheria ya Watu Wenye Ulemavu (Haki na Fursa Sawa) namba 9/2006, Sheria ya kuanzisha ofisi ya Mufti namba 9/2001, Sheria ya usajili wa nyumba na nyaraka sura ya 101/1926, Sheria ya Afya na Usalama Kazini 8/2005 na kusisitiza kuwa hizi ni baadhi tu ya sheria zilizofanyiwa mapitio

Waziri Khamis amesema Sekta ya Sheria imezidi kuimarika ambapo Serikali imeona umuhimu wa kuanzisha Idara ya Msaada wa Kisheria itakayoratibu utoaji na upatikanaji wa huduma ya kisheria kwa wananchi wote bila kujali uwezo wa kifedha kwa mtaka huduma.

Kuhusu Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Wizara imefanya utafiti wa kuzitambua nyaraka za mali za Wakfu na Amana zilizopotea, kujua wasia wa wakfu hizo, kuwatambua wanufaika halali pamoja na kuziweka taarifa hizo katika mfumo wa kieletroniki.

Hatua ambayo amesema imerahisisha utendaji na sasa wananchi wanapata huduma kwa urahisi zaidi, wapangaji wanapata mahali pazuri pa kuishi, kufanya biashara na ofisi zao na wanufaika halali wanapata haki zao kwa wakati unaostahiki.

Sekta ya Sheria Zanzibar imeimarisha ushirikiano baina yake na Sekta ya Sheria ya Jamhuri Muungano wa Tanzania, kushiriki katika shughuli za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, SADC, ushiriki katika Shirika la Mashauriano ya Sheria kwa Nchi za Asia na Afrika (Asia-African Legal, Consultative Organization (AALCO), ushiriki katika Umoja wa Tume za Kurekebisha Sheria za Afrika Mashariki na Kusini (ALRAESA) na Umoja wa Tume za Kurekebisha Sheria za nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CALRAs), Mahakama Kuu Zanzibar imefanikisha uenyeji wa mkutano wa Jumaiya ya Mahakimu na Majaji wa Afrika ya Mashariki .

Waziri Khamis pia aligusia mwelekeo wa baadae wa Wizara ambapo amesema pamoja na mafanikio hayo Wizara ya Katiba na Sheria imeweka muelekeo mzuri na inaendelea na hatua kuendeleza utekelezaji wa Sera, Sheria na Mipango ya kukuza upatikanaji wa haki ili kuimarisha uchumi wa Taifa.

Kuendeleza ujenzi wa Jengo la Mahakama Kuu Tunguu ikiwa ni katika vipaumbele vya kitaifa, Jengo ambalo litakapokamilika litapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la nafasi za Ofisi kwa Mhimili wa Mahakama na kuimarisha ufanisi kuitendaji;

Aidha uimarishaji uendeshaji wa Mashtaka kwa kesi za udhalilishaji wa kijinsia, madawa ya kulevya, makosa ya uhujumu wa uchumi na zile za kawaida ni moja kati ya vipaubele vya Wizara

Kuimarisha usimamizi wa mashauri ya madai kwa Mawakili wa Serikali katika masuala ya migogoro ya ardhi pamoja na kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali ili kuweza kushughulikia kitaalamu makosa ya jinai na madai yanayoibua changamoto kubwa kwa jamii.

Kuongeza kasi ya kufanya mapitio ya sheria kwa kutoa kipaumbele maalum kwenye Sheria za Ardhi.

Kusimamia na kuratibu shughuli za fatwa, mashauri, ushauri wa kidini, taaluma, tafiti, miskiti na madrasa, na kuimarisha huduma za Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana.

Waziri Khamis amesema zipo baadhi ya changamoto katika Wizara ikiwemo Uelewa mdogo wa wananchi kuhusiana na masuala ya Sheria na Ushirikiano mdogo kutoka kwa wananchi pale ambapo wanahusika kutoa ushahidi katika kesi mbalimbali na kuwasihi wananchi kutoa Ushirikiano pale inapohotajika kufanya hivyo

Mhe Khamis amemalizia na kusema kuwa mafanikio haya yanatokana na uongozi imara wa Dkt Shein ambapo viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na wafanyakazi wake wanaahidi kuendelea kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa majukumu yake kwa kushirikiana na wadau mbali mbali pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Huduma za Tehama

Barua Pepe Msaada wa kisheria

Sisi

Mwanzo Kuhusu Sisi Idara Zetu

Viunga Muhimu

MAHAKAMA DPP WAKFU LRC SADC IKULU

Mawasiliano

Ofisi Kuu
S.L.P 772, Mazizini, Zanzibar
Tel.: +255(24)2234683 Mhe Waziri



Tel.: +255 (24)2234684 Katibu Mkuu,
Fax: +255 (24)2234689
Email: info@sheriasmz.go.tz